Karibu

Habari yako? Na habari ya Tanzania? Salaam toka Welisi, UK.

Nimefurahi kuona kwamba umetafsiri jumbe zingine hapa. Nimeongeza taarifa ya kutafsiri katika Babel box yako na nimekuweka katika orodha ya watafsiri katika Portal:Sw. Usipopenda hivyo, futa tu.

Kama wewe ninatafsiri hapa ingawaje mimi si Mswahili. Ninatafsiri jumbe rahisi moja kwa moja. Lakini ninapokuwa na wasiwasi yeyote, ninaweka alama ya !!FUZZY!! mwanzoni kabisa. Jumbe hizi zinabaki hapa translatewiki.net, bila kupelekwa katika mradi unaohusika (Kiwix kwa mfano), hadi alama itakapotolewa. Halafu, ninaomba msaada wa Muddyb azitazame, kuzihariri na kuondoa !!FUZZY!!. Huwa inachukua muda hadi anapopata nafasi kuziangalia, shauri ya shughuli nyingi na kukosa umeme mara kwa mara. Lakini tumeweza kutafsiri namna hiyo, bila kuleta jumbe nyingi zilizo na makosa katika Mediawiki. Labda taratibu hii itakufaa wewe pia. Au labda unao wahariri kule unapoishi, unaoshauriana nao kabla ya kuweka tafsiri hapa. Bahati mbaya, sina mtu wa kushauriana naye hapa Ulaya.

Lloffiwr15:40, 24 September 2011